Sunday , September 23 2018
Home » Uncategorized » WABUNGE,MAWAZIRI FUATENI MIONGOZO YA BUNGE

WABUNGE,MAWAZIRI FUATENI MIONGOZO YA BUNGE

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali na wabunge wazingatie mwongozo uliowahi kutolewa na Spika wa Bunge, Job Ndugai unaowataka wabunge waulize maswali kwa ufupi na pia Serikali itoe majibu mafupi ya maswali ya msingi.

“Swali limeuliza lini majibu yake yanajaa ukurasa mzima, waheshimiwa wabunge nadhani wote tunajua, maswali ya nyongeza mtu anauliza dakika tatu swali la nyongeza, majibu kwa sababu tunapewa mapema tutayarishe hayo maswali kabisa kuliko unaenda unasema je,unaacha kwa sababu, unasema kwa nia, unasema tena je, sasa huelewi hayo ni maswali matatu au swali moja. Kwa hiyo waheshimiwa wabunge naomba tuzingatie huo mwongozo aliotoa Mheshimiwa Spika lakini pia Wizara zizingatie huo mwongozo wa kuleta majibu mafupi” amesema Dk. Ackson baada ya kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao cha 25 cha Mkutano wa 11 wa Bunge.

About PamojaFM

Check Also

Pwani Kibaha: Kibaka ajisalimisha kituo cha Polisi baada ya mzigo alioiba kumng’ang’ania kichwani

Mkazi wa Mbezi, Dar es salaam, Frank Japhet (23) amelazimika kujisalimisha kituo cha polisi Mlandizi, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *