Sunday , September 23 2018
Home » Uncategorized » MWIJAGE- HAKUNA UHABA WA SUKARI

MWIJAGE- HAKUNA UHABA WA SUKARI

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amelieleza Bunge kuwa, hakuna uhaba wa sukari Tanzania Bara.

Amesema, kuna tofauti ya bei ya bidhaa hiyo Tanzania bara na Zanzibar kwa kuwa, zaidi ya asilimia 53 ya sukari inayotumika Zanzibar inaagizwa kutoka nje kwenye vyanzo ambavyo gharama zake ni nafuu ukilinganisha na vile vya Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa Mwijage asilimia 29 ya sukari inayotumika Tanzania Bara inaagizwa kutoka nje na kwamba, Serikali imehamasisha na kusimamia kampuni nne zinazozalisha bidhaa hiyo zipanue uwezo wa mashamba na viwanda vyao.

“Lakini upande wa bara na nchi nyingine za Afrika Mashariki bidhaa ya sukari kutoka nje hutozwa ushuru kwa asilimia 100 ili kulinda viwanda vya ndani. Kutokana na sababu hizo bei huweza kutofautiana” amesema.

Ameyasema hayo wakati anajibu maswali ya Mbunge kutoka Baraza la Wawakilishi, Jaku Hashim Ayoub. Kwa mujibu wa Mbunge huyo, kuna viwanda vingi vya sukari nchini lakini kuna uhaba wa bidhaa hiyo hasa Tanzania Bara.

Ametoa mfano kwamba, sukari mfuko wa kilo 50 inauzwa sh 65,000/- Zanzibar na kuna kiwanda kimoja tu, lakini Tanzania Bara mfuko huo unauzwa sh 120,000/-.

Ayoub amehoji, kwa nini sukari inauzwa bei juu kiasi hicho Tanzania Bara na Serikali inachukua hatua gani ili wananchi wapate unafuu kuipata bidhaa hiyo.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo, wakati wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inashusha ushuru wa kuingiza sukari visiwani humo, kwa nini Serikali ya muungano nayo isifanye hivyo ili wananchi waipate bidhaa hiyo kwa bei nafuu.

About PamojaFM

Check Also

Pwani Kibaha: Kibaka ajisalimisha kituo cha Polisi baada ya mzigo alioiba kumng’ang’ania kichwani

Mkazi wa Mbezi, Dar es salaam, Frank Japhet (23) amelazimika kujisalimisha kituo cha polisi Mlandizi, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *