Sunday , September 23 2018
Home » Uncategorized » MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 800 KATIKA MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVI

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 800 KATIKA MANISPAA YA MPANDA MKOANI KATAVI

Na Mark Ngumba-Katavi.

JUMLA ya miradi 15 ya maendeleo katika halmashauri ya manispaa ya Mpanda imepitiwa na mwenge wa uhuru na kuzindua miradi 36 huku miradi 26 ikiwekewa mawe ya msingi.

Akizungumza katika makabidhiano ya miradi hiyo kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Charlse Francis Kabeho amesema serikali ya awamu ya tano chini rais dokta John Pombe Magufuli itaendelea kujenga miradi zaidi ili kusaidia upatikanaji wa huduma za kijamii kupatikana kirahisi kwa wananchi wake.

Miradi hiyo  iliyozunduliwa yenye thamani ya zaidi ya shilingi  milioni 800 ni pamoja na zahanati ya nilala,kisima cha maji milala na vyumba vitatu vya madarasa ya kisasa katika shule ya msingi nyerere.

Katika miradi hiyo wananchi wamechangia zaidi ya milioni miamoja kama mchango wa kujitolea kama sera ya maendeleo inavyowataka kuchangia asilimia 20% ya fedha au nguvu kazi katika miradi inayotekelezwa na serikali.

Katika hatua nyingine kiongozi huyo wa mbio za mwenge amewataka wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya vyandarua vinavyotolewa na serikali ili kujikinga na ugonjwa wa homa ya maralia.

Mwenge wa uhuru umewasili mkoani katavi  leo may 2018 na utakimbizwa kwa siku tano katika halmashauri zote za mkoa wa katavi ukitokea mkoani Tabora na kukimbizwa katika kata zote za manispaa ya Mpanda ambapo kesho utakabidhiwa katika halmashauri ya wilaya ya mlele.

About PamojaFM

Check Also

Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM Sumbawanga auawa kwa kupigwa risasi

Sumbawanga. Mtendaji wa Kata ya Mwandui iliyopo mwambao wa bonde la ziwa Rukwa, wilayani Sumbawanga …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *