Sunday , September 23 2018
Home » Habari » Watu watano wafariki katika ajali Morogoro.

Watu watano wafariki katika ajali Morogoro.

Watu watano, wanawake wanne na mwanaume mmoja wamepoteza maisha katika ajali iliyohusisha basi la New force T 346 DLY iliyokuwa ikitokea Dar kuelekea Tunduma na Hiace T 962 BSE iliyokuwa ikitokea kijiji cha Mlali kuelekea mjini Morogoro.

Ajali hiyo imetokea saa 4.15 asubuhi eneo la Lungenba, kilometa chache kutoka Msamvu kuelekea Iringa.

RTO wa mkoa wa Morogoro Boniphace Mbao amesema majeruhi wa ajali hiyo ni 12 ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro.

Chanzo cha ajali ni dereva wa Hiace kujaribu kuyapita magari mengine bila tahadhali na kwenda kugongana uso kwa uso na basi hilo.

Dereva wa Hiace amepoteza maisha.

About PamojaFM

Check Also

Mfanyabiashara Yusuf Manji baada ya kuachiwa huru na Mahakama leo.

Ijumaa October 6, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *